IQNA

Wanaharakati 60 wa masuala ya Qur'ani kuenziwa mjini Makka

17:34 - October 17, 2011
Habari ID: 2206688
Shakhsia 60 wanaojishughulisha na masuala ya Qur'ani wataenziwa kesho kutokana na hima na juhudi za Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'ani ya Makka Tukufu.
Shakhsia hao 60 wataenziwa kesho katika sherehe ya kutimia mwaka wa 50 tangu kuasisiwa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'ani Tukufu ya Makka kutokana na juhudi zao kubwa katika kuhudumia mafunzo ya Qur'ani Tukufu.
Sherehe hiyo itahudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa Saudia akiwemo Waziri wa Masuala ya Kiislamu na maulamaa wa nchi hiyo.
Vilevile katika sherehe hiyo kutazinduliwa kitabu makhsusi kinachoelezea historia ya shughuli za Kiqur'ani za taasisi hiyo ambayo ni kwanza kabisa ya Qur'ani kuasisiwa nchini Saudi Arabia. 881462
captcha