IQNA

12:57 - October 20, 2011
Habari ID: 2208406

Ushindi wa Hamas katika kubadilishana mateka unatokana na mapambano ya Wapalestina

Khalid Mash'al, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amesema kwamba ushindi wa hivi karibuni wa harakati hiyo katika kubadilishana mateka na utawala haramu wa Israel unatokana na mapambano na subira ya taifa shupavu la Palestina.

Amesema kubadilishana idadi kubwa ya mateka wa Palestina na askari jeshi mmoja tu wa utawala haramu wa Israel ni ushindi mkubwa unaotokana na juhudi, mapambano makali na busara kubwa ya kiusalama iliyoonyeshwa na Wapelestina.
Mash'al amesema kwamba madai ya Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Utawala wa Israel kwamba Hamas inazidi kudhoofika yamekadhibishwa na kujibiwai na ushindi mkubwa wa hivi karibuni wa Hamas katika ubadilishaji huo wa mateka, jambo ambalo amesema limekuwa ni jibu la kuufedhehesha utawala huo ghasibu.
Akizungumzia suala hilo pia Ismail Hania Waziri Mkuu wa serikali ya Palestina amesema kuwa mapambano ndiyo njia pekee ya kukabiliana na utawala haramu wa Israel na kwamba hiyo ndiyo mbinu iliyotumika katika kuwafukuza wavamizi wa Kizayuni katika ardhi ya Ukanda wa Gaza.
Amesema mapambano ndiyo siri ya kukombolewa ardhi na mateka wa Kipalestina na kuwa nguvu ya mapambano imethibiti katika kutekwa kwa muda wa zaidi ya miaka mitano Gilad Shalit, askari jeshi wa utawala wa Israel na kufichwa katika Ukanda wa Gaza katika kipindi hicho chote, ukanda ambao utawala huo unadai kwamba unaudhibiti kikamilifu katika mtazamo wa kiusalama. 882943
captcha