IQNA

Maonyesho ya nuskha za maandishi ya mkono ya Kiislamu na Qur'ani yafanyika New York

16:25 - October 22, 2011
Habari ID: 2209386
Maonyesho ya 'Hazina ya Uchoraji na Uandishi wa Mkono wa Kiislamu' yanayojumuisha nuskha na hati za Kiislamu na Qur'ani yalianza jana Ijumaa katika jumba la maonyesho ya mambo ya kale na maktaba ya mjini New York.
Kwa mujibu wa tovuti ya Islam Today, vitabu, maandiko na hati za zamani za Kiislamu zaidi ya 90, zikiwemo za Qur'ani na kaligrafia ya Kiislamu zinaonyeshwa katika maonyesho hayo.
Baadhi ya hati za kale zinazoonyeshwa kwenye maonyesho hayo ni pamoja na Qur'ani iliyoandikwa kwa mkono mwaka 1580 Milaadia katika mji wa Shiraz nchini Iran. Qur'ani hiyo ilitolewa kama zawadi na Mfalme Ahmad III mwanzoni mwa muongo wa 1700 kwa Msikiti wa Jarah Basha.
Umuhimu wa Qur'ani hiyo iliyoandikwa kwenye ngozi unadhihiri pale tunapotilia maanani ukweli kwamba imewekwa mwanzoni mwa ukumbi wa maonyesho hayo ambayo yanajumuisha nuskha nyinginezo za kitabu hicho cha mbinguni.
Kazi ya kufanyia nakshi kwa dhahabu Qur'ani Tukufu iliyofanywa na Jalal Deen Muhammad Rumi pia inaonyeshwa kwenye maonyesho hayo ambayo yamepangwa kuendelea hadi 28 Februari. 884244
captcha