Gazeti la al Riyadh limeandika kuwa mpango huo ni moja ya miradi ya elimu ya Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Riyadh ambapo kwa mujibu wake washiriki watahifadhi Qur'ani nzima katika kipindi cha miaka mitatu.
Mkurugenzi wa Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Kuhifadhisha Qur'ani Tukufu ya Riyadh Sheikh Ibrahim bin Abdullah amesema kuwa mpango huo utawashirikisha wanafunzi watakaopewa masomo makhsusi ya kuhifadhi Qur'ani.
Amesema kundi la walimu wenye ozoefu litatumiwa kutoa mafunzo ya kuhifadhi Qur'ani kwa wanafunzi hao. Ameongeza kuwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika mpango huo watapewa zawadi ya riyale 1500 na kuiwakilisha jumuiya hiyo katika mashindano ya kitaifa na kimataifa ya Qur'ani Tukufu. 884734