Katika kipindi ambacho utawala haramu wa Israel unafanya mjama za kupotosha historia ya Kiislamu ya mji wa Quds Tukufu huko Palestina kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchoma moto nakala za Qur'ani ndani ya misikiti, gazeti la Haaretz la Israel limetangaza kuwa maonyesho ya nuskha za kale za Qur'ani Tukufu yanafanyika katika mji huo.
Toleo la jana la gazeti la Haaretz liliandika kuwa Maktaba ya Taifa ya Israel itafanya maonyesho ya nakala za kale na kihistoria za Qur'ani Tukufu katika mji wa Quds. Maonyesho hayo yanafanyika leo.
Maktaba ya Taifa ya Israel ambayo imeamua kuchukua hatua hiyo kwa lengo la kuwahadaa Waislamu, itaonyesha nakala mbili za Qur'ani zilizoandikwa katika karne ya 9 Miladia, na nakala nyingine tatu za kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu za karne ya 11 na 12 zilizotolewa katika miji ya Andalusia huko Uhispania na Antakya nchini Uturuki.
Pambizoni mwa maonyeho hayo, utawala wa Kizayani wa Israel utafanya vikao kuhusu historia ya Uislamu.
Maonyesho hayo ya vitabu yanaonyeshwa na utawala ghasibu wa Israel katika hali ambayo jeshi la nchi hiyo na walowezi wa Kizayuni wanaendelea kushambulia na kuchoma moto misikiti na Qur'ani Tukufu katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina. 885622