IQNA

Mashindano ya Qur'ani kufanyika Brunei

17:26 - October 24, 2011
Habari ID: 2211060
Mashindano ya kiraa ya Qur'ani Tukufu yatafanyika tarehe 1 Novemba nchini Brunei.
Mashindano hayo yanayosimamiwa na Ofisi ya Jumuiya ya Masuala ya Misikiti yatafanyika katika maeneo manne ya nchi hiyo.
Mashindano hayo yaliyotayarishwa na Wizara ya Masuala ya Kidini yatakuwa na pande mbili za wanaume na wanawake na yatawashiriki makarii kutoka maeneo yote ya Brunei.
Washindi watawakilishi nchi hiyo katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yatakayofanyika Kuala Lumpur. 885431


captcha