Msemaji wa chuo hicho amesema kuwa nakala hiyo iliyoandikwa kwa hati za mkono ni miongoni mwa nuskha nadra na muhimu mno za Qur'ani duniani.
Ameongeza kuwa nalaka hiyo pamoja na nakshi zake iliandikwa kwa hati za mkono miaka 500 iliyopita na haijawahi kuonyeshwa hata mara moja kutokana na ulaini na muundo wa karatasi zake.
Msemaji wa Chuo Kikuu cha Manchester amesema kuwa nakala hiyo nadra ya Qur'ani Tukufu ina kurasa 470 na inahifadhiwa katika maktaba ya chuo hicho.
Licha ya hitilafu zilizopo kati ya wanahistoria kuhusu historia ya kuandikwa Qur'ani hiyo, taarifa zilizopatikana zinaonyesha kuwa nakala hiyo iliandikwa katika karne ya 14 au 15 Miladia. 887855