IQNA

Misimamo ya Wakristo kuhusu Qur'ani kuchunguzwa Tennessee

12:42 - October 27, 2011
Habari ID: 2212706
Kikao cha kuchunguza misimamo ya Wakristo kuhusu kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika kipindi chote cha historia kitafanyika Jumamosi ijayo katika Chuo Kikuu cha Tennessee nchini Marekani.
Kikao hicho kitahudhuriwa na wasomi na wahadhiri wa vyuo vikuu akiwemo Tomm Bremen, mhadhiri katika chuo Kikuu cha Tennessee.
Msomi huyo atahutubia kuhusu misimamo ya Wakristo juu ya kitabu kitakatifu cha Waislamu katika kipindi chote cha historia.
Amesema atatoa mifano kuhusu historia ya kipindi cha karne za kati ambapo Wakristo wa Ulaya walikuwa wakikiona kitabu cha Qur'ani kuwa ni hatari kubwa na walikuwa wakiamiliana na kitabu hicho kutokana na taswira hiyo.
Msomi huyo pia atachunguza miamala ya kidini na kifikra kati ya Wakristo na Waislamu hususan tarjumi za vitabu vya Kiarabu na Kiislamu zilizofanywa barani Ulaya katika karne za kati.
Vilevile atachunguza uhusiano wa Waislamu na Wakristo na Wayahudi, Vita vya Msalaba na kadhalika. 887523


captcha