IQNA

Nyumba za Qur'ani kuanzishwa katika vyuo vikuu nchini Iran

12:41 - October 27, 2011
Habari ID: 2212709
Naibu Waziri wa Elimu wa Iran amesema kuwa wizara hiyo imepasisha suala la kuanzishwa Nyumba ya Qur'ani katika vyuo vikuu kote nchini.
Vituo hivyo vitasimamia shughuli zote zinazohusiana na Qur'ani.
Ghulamreza Khajesaravi amesema kuwa viongozi wa Wizara ya Elimu, Uhakiki na Teknolojia wamepasisha kuanzishwa Nyumba ya Qur'ani katika vyuo vikuu katika juhudi za kuzidisha nafasi ya kitabu hicho kitakatifu katika harakati za vyuo hivyo.
Naibu Waziri wa Elimu wa Iran ameongeza kuwa zinafanyika juhudi kubwa kuhakikisha kwamba shughuli zote za kielimu katika vyuo vikuu zinafanyika kwa mujibu wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu ya Ahlul Bait wa Mtume Muhammad (saw). 887503



captcha