IQNA

Mashindano ya hifdhi ya Qur'ani kufanyika katika Mkoa wa Dhi Qar nchini Iraq

12:48 - October 27, 2011
Habari ID: 2212710
Idara ya elimu na malezi ya Mkoa wa Dhi Qar ulioko kusini mwa Iraq imeandaa mashindano ya hifdhi na tajwidi ya Qur'ani Tukufu ambayo yamepangwa kuzishirikishja shule zote za msingi za mkoa huo.
Rad Adnan an-Nassiri, msimamizi wa masuala ya uratibu katika Kamati Kuu ya Qur'ani Tukufu ya Baraza la Mawaziri la Iraq katika Mkoa wa Dhi Qar ambaye pia ni mkuu wa Taasisi ya Dar al-Qur'an al-Karim katika mji wa Nassiria amewaambia waandishi habari kuhusiana na suala hilo kwamba idara ya elimu na malezi ya mkoa huo inafanya juhudi kubwa za kufanikisha mashindano hayo muhimu ambayo yamepangwa kufanyika wiki ijayo.
Amesema mashindano hayo yatawashirikisha wanafunzi wa kike na kiume wa shule za msingi katika mkoa uliotajwa.
Rad Adnan amesema mashindano hayo ambayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka yatahusisha hifdhi ya juzuu tano hadi ishirini za Qur'ani. 887565
captcha