IQNA

Washindi wa mashindano ya hifdhi ya Qur'ani kwa walemavu wa akili nchini Misri kuenziwa

11:20 - October 30, 2011
Habari ID: 2214184
Washindi wa mashindano ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu makhsusi kwa walemavu wa akili nchini Misri wataenziwa baada ya kumalizika sikukuu ya Idul Adh'haa.
Sherehe za kuwaenzi washindi hao zimeandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri. Hatua ya amwisho ya mashindano hayo ilifanyika siku ya Alkhamisi ambapo washiriki 60 wa mashindano hayo waliteuliwa kuwa washindi wa mwisho.
Washindi hao ni pamoja na washiriki 10 walioshinda katika kundi la hifdhi ya robo moja ya Qur'ani, 20 walioshinda hifdhi ya juzuu moja ya Qur'ani na 30 wa mwisho ni wale walioshinda katika hifdhi ya baadhi ya aya za kitabu hicho cha mbinguni.
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri awali ilikubali kuongeza nambari ya washindi wa mashindano hayo kutoka watu 30 hadi 60. Imekubali pia kuongeza zawadi ya washindi kutoka juneih 10,000 hadi juneih 20,000. 889119
captcha