IQNA

16:24 - November 01, 2011
Habari ID: 2215774

Saudia yamwachilia huru hujaji wa Kishia raia wa Canada

Utawala wa Saudi Arabia ulimwachilia huru jana Jumatatu hujaji mmoja wa Kishia ambaye ni raia wa Canada.

Utawala huo ulikuwa umemtia nguvuni hujaji huyo kwa jina la Usama al-Attar kwa kosa la kukosoa itikadi na sera za Mawahabi katika mji mtakatifu wa Madina.
Askari wa Saudia walimtia nguvuni hujaji huyo siku ya Jumapili baada ya kukosoa katika mji mtakatifu wa Madina, itikadi na siasa za utawala wa Kiwahabi. Utawala huo umelazimika kumwachilia hujaji huyo baada ya ubalozi wa Canada nchini Saudia kutoa mashinikizo ya kutaka aachiliwe huru.
Usama al-Attar ambaye ana umri wa miaka 33 ni mtafiti katika Chuo Kikuu cha Alberta nchini Canada. Amesema, baada ya kutiwa nguvuni aliteswa na kutukanwa na askari usalama wa Saudia. Muhammad Hayward, mmoja wa mahujaji ambaye alishuhudia tukio hilo amesema kuwa polisi 15 wa Saudia walimtia nguvuni al-Attar aliyekuwa akiwahutubia wenzake na kumpiga kabla ya kumchukua na kwenda naye sehemu isiyofahamika.
Hujaji huyo alitazamiwa kuhukumiwa jana lakini utawala wa Saudia ulilazimika kumwachilia huru baada ya kuakisiwa suala hilo na vyombo vya habari vya kimataifa, Baraza la Kutetea Haki za Binadamu la Kiislamu la Uingereza na mashinikizo yaliyotolewa na ubalozi wa Canada nchini humo. 891103
captcha