IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kufanyika Canada

19:37 - November 02, 2011
Habari ID: 2216689
Mashindano ya kimataifa ya kiraa ya Qur'ani Tukufu yatafanyika tarehe 19 Novemba katika mji wa Toronto nchini Canada kwa hima ya Jumuiya ya Imam Ridha (as).
Kituo cha Imam Reza Circle kimeripoti kuwa sehemu ya hifdhi ya mashindano hayo itakuwa na makundi matatu ya hifdhi ya juzuu ya 30 ya Qur'ani kwa watu wenye umri wa miaka 10, hifdhi ya nusu ya Qur'ani Tukufu kwa watu wenye umri wa miaka 11 hadi 15, na hifdhi ya Qur'ani nzima kwa wale wenye umri wa juu ya miaka 16.
Sehemu ya kiraa ya mashindano hayo haitakuwa na kizuizi cha umri na kila mshiriki atapewa aya atakazozisoma dadika 10 kabla ya kutahiniwa.
Mashindano hayo yatahudhuriwa na jumuiya mbalimbali za Kiislamu nchini Canada.
Tarehe 22 mwezi uliopita wa Oktoba Jumuiya ya Kiislamu ya Imam Ridha (as) pia ilitayarisha mashindano ya Qur'ani ya wanawake Waislamu wa Canada. 892025
captcha