IQNA

Rais Ahmadinejad:

Kasi ya mwamko wa kuhifadhi Qur'ani inapaswa kuongezwa

15:22 - November 06, 2011
Habari ID: 2218512
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametaka harakati na mwamko wa kuhifadhi Qur'ani nchini Iran uongezewe kasi.
Amesema hayo katika sherehe maalumu za kuanza kampeni ya kuhifadhi Qur'ani nchini Iran na kusisitiza kuwa, utawala wa Mwenyezi Mungu duniani uliosimama juu ya uadilifu, upendo na ubinadamu utadumishwa tu kwa kuelewa vizuri na kutekelezwa ipasavyo mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Amesema kuwa, kuyatambua vizuri mafundisho ya Qur'ani na kutekeleza kivitendo yote yaliyomo kwenye Kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu ndiyo njia iliyonyooka na kwamba mtu yeyote asiyefuata njia hiyo atapotea na kamwe hatapata mafanikio ya kweli katika mambo yake.
Rais Ahmadinejad ameongeza katika sherehe hizo za kuanza harakati ya taifa ya kuwahifadhisha Qur'ani Tukufu wanafunzi wa shule za msingi nchini Iran kwamba, inabidi harakati hiyo iendelee kwa kasi kubwa katika kila kona ya Iran ya Kiislamu ili baraka za Mwenyezi Mungu zizidi kushuhudiwa hapa nchini. 893743
captcha