IQNA

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu kufanyika Ubelgiji

20:20 - November 06, 2011
Habari ID: 2218544
Mashindano ya kitaifa ya usomaji Qur'ani Tukufu kwa watoto wasio na walinzi yamepangwa kufanyika Brussels mji mkuu wa Ubelgiji hapo tarehe 19 Novemba.
Kwa mujibu wa tovuti ya irbelgium mashindano hayo yanadhaminiwa na tawi la Ubelgiji la Taasisi ya Kimataifa ya Misaada ya Kiislamu.
Watoto wote wasio na walezi kutoka kila pembe ya nchi hiyo wamealikwa kushiriki. Mashindano ya utangulizi ya mashindano hayo ya kitaifa yatafanyika tarehe 12 Novemba katika miji tofauti ya nchi hiyo na washindi kuchaguliwa ili kushiriki katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo.
Waislamu wote wa Ubelgiji wameombwa kufika katika ukumbi wa Lumen ili kushangilia na kuwashajiisha watoto hao ili kwa njia hiyo nao wapate kuwashawishi watoto wao wenyewe wawezi kusoma na kuhifadhi Qur'ani.
Vilevile misaada ya wananchi itakusanywa pambizoni mwa mashindano hayo ili kuwasaidia watoto wasio na walezi na pia familia zinazohitaji misaada ya Waislamu wenzao. 894085
captcha