IQNA

Zaidi ya nuskha milioni tatu za Qur'ani zatawanywa miongoni mwa Mahujaji

16:40 - November 08, 2011
Habari ID: 2219276
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu na Tablighi ya Saudi Arabia imetawanya zaidi ya nushkha za Qur'ani milioni tatu ambazo zimetarjumiwa kwa lugha tofauti miongoni mwa mahujaji ambao hivi sasa wako nchini humo kwa ibada tukufu ya hija.
Kwa mujibu wa gazeti la at-Riyadh la Saudia, nuskha hizo za Qur'ani zimechapishwa na Taasisi ya Uchapishaji na Usambazaji wa Qur'ani Tukufu ya Mfalme Fahd katika mji mtakatifu wa Madina na kusambazwa miongoni mwa mahujaji wa nchi tofauti.
Qur'ani hizo ambazo huchapishwa kwa lugha tofauti hutolewa kila mwaka kwa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu. 894693
captcha