IQNA

Mashindano ya hifdhi na usomaji Qur'ani Amerika Kaskazini kufanyika

16:41 - November 08, 2011
Habari ID: 2219278
Duru ya saba ya mashindano ya kila mwaka ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu ya Amerika Kaskazini yamepangwa kufanyika mwezi Machi mwakani.
Mashindano hayo yanadhaminiwa na Taasisi ya Kiislamu ya Toronto. Kwa mujibu wa tovuti ya Qiraat Competition mashindano hayo yatafanyika katika makundi tofauti ya wanawake na wanaume ambapo ya wanawake yamepangwa kufanyika tarehe Tatu Machi na ya wanaume tarehe 9 hadi 12 Machi.
Vijana wa kiume walio na umri wa miaka 22 watashindana katika makundi matatu ya hifdhi ya Qur'ani nzima, hifdhi ya juzuu ya 6 hadi 15 ya Qur'ani Tukufu na hifdhi ya juzuu ya kwanza hadi 6 ya kitabu hicho kitakatifu. Makundi mengine ya wanaume na wanawake yamepangiwa kushiriki katika makundi tofauti ya hifdhi na kiraa ya Qurani Tukufu.
Washiriki wa mashindano hayo watasimamiwa na waamuzi mashuhuri wa Qur'ani na mwishowe washindi watatu kutoka kila kundi shiriki watachaguliwa kuwa washindi wa mwisho na kutunukiwa zawadi nono.
Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na taasisi iliyotajwa kwa lengo la kuwashajiisha vijana wahifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu kwa lengo la kuandaa uwanja wa kuwavutia vijana wa Kiislamu wa Amerika Kaskazini kufungamana zaidi na kitabu hicho cha mbinguni. 894334
captcha