IQNA

15:58 - November 09, 2011
Habari ID: 2219603

Uingiliaji wa kijeshi Syria utahatarisha usalama wa nchi za Magharibi

Mufti Mkuu wa Syria ametahadharishi dhidi ya uingiliaji wa kijeshi wa shirika la kujihami la nchi za Magharibi Nato nchini Syria na kusema kuwa jambo hilo litakuwa na athari nyingi mbaya kwa nchi za Ulaya na Magharibi kwa ujumla.

Sheikh Badrideen Hassun ameonya kwamba iwapo nchi hizo zitaishambulia Syria Wasyria watazisababishia matatizo mengi na hatari. Amesema iwapo mashambulio kama hayo yatafanyika si Wasyria tu bali Waislamu wote watashiriki katika operesheni za kuzisababishia nchi za Magharibi matatizo ya kiusalama.
Huku akisisitiza kwamba Rais Bashar al-Assad ana azma madhubuti ya kufanya marekebisho ya kisiasa nchini humo amesema kwamba Jumuiya ya Nchi za Kiarabu haina uwezo wa kutatua matatizo ya ndani ya Syria.
Amezitaka nchi za Ulaya kuwajibika kuhusiana na Syria na kuongeza kuwa nchi hizo zinaweza kuwa na nafasi muhimu nchini humo iwapo zitawajibika na kutekeleza majukumu yao ipaswavyo. Amesema umoja wa Ulaya una nafasi muhimu katika kutatua matatizo ya Syria kuliko Jumuiya ya Nchi za Kiarabu inayoathiriwa na siasa za Marekani.
Wakati huohuo amezionya nchi za Ulaya na Marekani kwamba iwapo zitathubutu kuishambulia kijeshi Syria basi zifahamu kuwa katika nchi hizo kuna watu ambao wako tayari kutekeleza operesheni za kujitolea kufa shahidi ambao watazisababishia matatizo makubwa ya kiusalama.
Sheikh Hassun ndiye kiongozi wa ngazi za juu zaidi katika masuala ya kidini nchini Syria ambaye ana uhusiano wa karibu na Ras Bashar al-Assad. Hivi karibuni mwanaye wa kiume aliuawa na magenge ya kigaidi yanayobeba silaha dhidi ya serikali. 894845
captcha