IQNA

Tamasha ya watoto ya kila mwaka ya Qur'ani Marekani

16:24 - November 12, 2011
Habari ID: 2221121
Tamasha ya kila mwaka ya kimataifa ya Qur'ani maalumu kwa watoto itafanyika tarehe 18-22 Aprili mwakani katika Taasisi ya Kiislamu ya Villa Park katika jimbo la Illinois.
Kwa mujibu wa tovuti ya ifsvp, tamasha hiyo ya siku tano inalenga kuarifisha mafundisho ya zama zote ya Qur'ani Tukufu na kuandaa mazingira ya watoto kudiriki kwa karibu ujumbe wa kimataifa wa Qur'ani Tukufu.
Katika tamasha hiyo kutakuwepo pia mashindano ya kuhifadhi Qur'ani yenye lengo la kuwatia motisha watoto wahifadhi zaidi Qur'ani Tukufu.
Washiriki watatahiniwa kuhusu uwezo wa kuhifadhi kikamilifu, uzingatiaji tajwidi na uzingatiaji ujumbe wa aya wanazosoma.
897053
captcha