Mshauri wa Waziri wa Wakfu wa Saudia Talal bin Ahmad Akiil amesema nakala hizo za Qur'ani na vitabu vya kidini zimetolewa kwa mahujaji katika viwanja vya ndege wakati wanapokuwa wakirejea nchini kwao.
Amesema katika kipindi chote cha ibada ya hija nakala laki mbili na nusu za Qur'ani Tukufu, tarjumi yake kwa lugha mbalimbali na vitabu vya kidini zilikuwa zikitolewa kila siku kwa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu. 897197