Raad Adnan ambaye ni Mratibu wa Kamati Kuu ya Qur'ani Tukufu ya Iraq katika mkoa wa Dhiqar amesema vikao na makongamano hayo ya Qur'ani yatafanyika katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya Ghadir katika mikoa mbalimbali ya Iraq.
Amesema kuwa vikao hivyo vya kiraa ya Qur'ani vinafanyika kwa kutilia maanani hadithi ya Bwana Mtume (saw) ambaye amesema: "Ali yuko pamoja na Qur'ani, na Qur'ani iko pamoja na Ali, na viwili hivyo havitatengana hadi vitakaponikuta mimi katika hodhi ya Kauthar."
Siku ya terehe 18 Dhulhija ni sikukuu ya Ghadir ambamo Waislamu wafuasi wa Ahlul Bait hukumbuka tukio la kutawazwa rasmi Ali bin Abi Twalib (as) kuwa Imam na kiongozi wa Waislamu wote baada ya Mtume (saw). 896958