Akizungumza katika kikao cha wataalamu katika Kongamano la Pili la Kimataifa la Wachapishaji wa Kiislamu mjini Tehran, Bw. Adel Ahmad Abdulmajid ameongeza kuwa, 'Tunachopaswa kufanya si kupunguza uchapishaji Qur'ani bali ni kujaribu kujibu maswali na tashwishi zinazoibuliwa na maadui".
Ameashiria nafasi ya wachapishaji na kusema wachapishaji katika ulimwengu wa Kiislamu wana jukumu kubwa la kueneza fikra na thamani za Kiislamu.
Akizungumza katika kongamano hilo pia, Ali Abul Khayr, mtaalamu wa Qur'ani kutoka Syria amesema Qur'ani Tukufu ni chanzo cha heshima katika umma wa Kiislamu. Amesema umoja wa Kiislamu ndio changamoto kubwa na kuongezwa kuwa madola ya kibeberu yanajaribu kupiga vita mafundisho ya Qur'ani kupitia njia ya kuzusha mifarakano miongoni mwa Waislamu.
897369