IQNA

Programu ya tarjumi ya Qur'ani kwa lugha ya Kisweden yazinduliwa

11:46 - November 14, 2011
Habari ID: 2222411
Mtandao wa intaneti wa http://android-apps.com umetengeneza programu ya Qur'ani ambayo ina sifa makhsusi ikiwa ni pamoja na kutarjumu Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kisweden.
Kwa mujibu wa tovuti ya android-apps.com, programu hiyo iliyotayarishwa kwa ajili ya simu za mkononi, inajumuisha matini kamili ya Qur'ani Tukufu kwa hati za Othman Taha na kiraa ya Qur'ani ya makarii 8 mashuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu.
Programu hiyo inaweza kutumiwa katika simu za mkononi zinazotumia sistimu ya Android.
Kisweden ni moja ya lugha za Ulaya ambayo pia inatumika katika nchi ya Finland. 898253
captcha