IQNA

Nigeria yatakiwa kuainisha siku makhsusi ya Qur'ani Tukufu

14:06 - November 14, 2011
Habari ID: 2222569
Kiongozi wa Kiislamu wa Nigeria amesema katika ufunguzi wa mashindano ya kitaifa ya kiraa ya Qur'ani kwamba kuna haja ya kutangazwa siku ya taifa ya Qur'ani nchini humo.
Ismail Abdullahi ambaye ni miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa Kiislamu nchini Nigeria amesema katika sherehe za ufunguzi wa mashindano ya 6 ya Qur'ani Tukufu katika jimbo la Jigawa kwamba viongozi wa serikali wanapaswa kutangaza siku ya taifa ya Qur'ani ambayo ndani yake kutafanyika kisomo cha Qur'ani Tukufu nchini kote.
Amesema kuwa kuainishwa siku kama hiyo kutawahamasisha vijana kutenga wakati wao kwa ajili ya kusoma Qur'ani, suala ambalo litakuwa na taathira chanya katika jamii.
Mashindano ya taifa ya Qur'ani Tukufu hufanyika kila mwaka nchini Nigeria kwa lengo la kuhamasisha vijana wa Kiislamu kuhifadhi na kusoma kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu, kuimarisha umoja baina ya Waislamu katika nyanja zote na kuboresha usomaji Qur'ani katika madrasa na vyuo vikuu nchini humo. 897962
captcha