Salah Sultan amesema kuwa maandamano hayo yatafanyika kwa ushirikiano wa Kamati ya Quds ya Jumuiya ya Madaktari wa Kiarabu.
Ameongeza kuwa juhudi zinafanyika kwa kushirikiana na Sheikh wa al Azhar Ahmad Tayyib na Mwenyekiti wa Muungano wa Maulamaa Waislamu Duniani Sheikh Yusuf Qaradhawi ili mmoja wa shakhsia hao aongoze maandamano hayo ya mamilioni ya watu ya kupinga ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina.
Amesema kuwa vyama mbalimbali vya siasa pia vitashiriki katika maandamano hayo.
Salah Sultan amesema kuwa Jumuiya ya Maulamaa Waislamu Duniani inatayarisha fatuwa na kuhalalisha damu ya Wazayuni kutokana na kuendelea kuifanya Quds kuwa ya Kiyahudi na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu. 898446