Kwa mujibu wa gazeti la Al Ettehad mashindano hayo yanafanyika chini ya usimamizi wa Sheikh Sa’ud bin Saqar Al-Qasimi, mtawala wa Ras Al-Khaimah.
Umar bin Abdul Aziz Al-Ghasemi, Katibu Mkuu wa mashindano hayo ambaye pia ni mkuu wa Taasisi ya Qur’ani ya Ras Al Khaimah amesema mashindano hayo yatajumuisha vitengo vya kuhifadhi Qur’ani kamili, juzuu 20,10, 5 na 3. Aidha kutakuwa na mashindano ya tajweed na tarteel.
Mashindano hayo yanatazamiwa kumalizika Novemba 24.
897624