IQNA

Aya 400 zinazohusu afya katika Qur’ani Tukufu

16:14 - November 16, 2011
Habari ID: 2223375
Katika Qur’ani Tukufu kuna karibu aya 400 zinazohusiana na afya, lishe na tiba, amesema mtaalamu wa masuala ya tiba ya Kiislamu nchini Iran.
Ahmad Mohammadian, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Razavi nchini Iran amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa wataalamu wanaweza kunufaika sana na aya hizi pamoja na hadithi zinazohusiana na masuala ya tiba.
Ameongeza kuwa watafiti katika uga wa tiba ya Kiislamu wanapaswa kuwa na ujuzi kuhusu sayansi za Kiislamu, lugha ya Kiarabu na taaluma ya hadithi.
Mohammadian amesema Kituo cha Utafiti wa Tiba ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Razavi kilianzishwa kwa lengo la kustawisha nadharia za Kiislamu katika tiba na lishe na kuelimisha umma kuhusu misingi ya afya kwa mujibu wa Ahlul Bayt AS na kuinua kiwango cha afya ya umma. 898804
captcha