IQNA

Mufti Msaudi akiri:

Qur'ani ni shifaa hata kwa wasiokuwa Waislamu

19:24 - November 16, 2011
Habari ID: 2223553
Mufti wa Kisaudi Arabia amekiri kwamba kitabu kitakatifu cha Qur'ani ni shifaa hata kwa Wasiokuwa Waislamu.
Fatuwa ya mufti huyo wa Kisaudia imeunga mkono mtazamo wa maulamaa wa Kishia ambao siku zote wamekuwa wakisisitiza kutokana na mafundisho ya Maimamu kutoka katika kizazi cha Mtume Muhammad (saw), kwamba Qur'ani Tukufu ni shifaa na rehma si kwa watu wa kaumu na kundi makhsusi bali wanadamu wote.
Sheikh Ali bin Ghazi al Tuwaijri alisema juzi katika kikao kilichofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Madina Tukufu kwamba inajuzu kwa wasiokuwa Waislamu kutafuta shifaa na ponyo ya matatizo na maradhi yao kwa kutumia kitabu cha Qur'ani Tukufu.
Sheikh al Tuwaijri amesema kujitibu kwa kutumia Qur'ani Tukufu ni miongoni mwa Suna za Mtume Muhammad (saw) na maulamaa wanakutambua kuwa ni Suna. Amesisitiza kuwa kitendo hicho si nakisi au aibu bali ni ukamilifu wa imani.
Sheikh Ali bin Ghazi al Tuwaijri amesema Qur'ani Tukufu ni shifaa na ponyo ya maradhi na matatizo ya kiroho na kimwili na haya yamethibitishwa katika aya za kitabu hicho na hadithi za Mtume Mtukufu.
Fatuwa hii inapingana na mafundisho na mitazamo ya Kiwahabi na kuunga mkono mtazamo wa maulamaa wa madhehebu ya Shia wanaotilia mkazo umuhimu wa kutafuta shifaa kwa kutumia maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu. 899255

captcha