Maonyesho hayo yamefanyika katika ukumbi wa Kituo cha Kiislamu cha Al Zahra katika mji wa Richmond huko British Colombia.
Kwa mujibu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu la Iran ICRO maonyesho hayo yaliyokuwa na anwani ya ‘Haram Asemani’ au Haram ya Mbinguni, yalifanyika Novemba 11 kwa ushirikiano wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Canada.
Kazi za sanaa kama vile kaligrafia ya Qur’ani, Majina ya Allah (Asmaul Husna) picha za Haram ya Imam Reza AS na picha za usanifu majengo wa Kiislamu zilionyeshwa katika maonyesho hayo.
Waislamu wa Canada na nchi kama vile Iran, Afghanistan, Pakistan, Iraq, Lebanon , Afrika Mashariki pamoja na mataifa mengine walihudhuria maonyesho hayo na kushiriki katika sala ya Ijumaa katika msikiti wa kituo hicho.
899281