Akizungumza katika Kongamano la Tisa la Kimataifa la Watafiti Wanawake katika uga wa Qur’ani, Bi. Amina Nassir ameongeza kuwa wanawaka wana majukumu mbalimbali katika jamii ikiwemo kuwa mke na mama ambaye analea kizazi kijacho.
Amesema kuwa Uislamu umeshawapa wanawake haki zao zote katika majukumu yao mbalimbali.
‘Uislamu uliinua hadi ya mwanamke na kumpa haki zake. Dini hii tukufu iliondoa fikra zote za kumdunisha mwanamke’. Ameelezea masikitiko yake kuwa katika baadhi ya sehemu za dunia wanawake bado wanadhulumiwa.
Bi. Nassir pia amewapongeza wanawake wa Iran kutokana na mafanikio makubwa waliyoweza kuyapata baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Mnara wa Milad mjini Tehran Alkhamisi Novemba 17.
899954