IQNA

Olimpiadi ya Qur’ani katika Chuo Kikuu cha Al Mustafa nchini Iran

14:31 - November 20, 2011
Habari ID: 2225101
Awamu ya 17 ya Olimpiadi ya Kimataifa ya Qur’ani kuhusu tafsiri ya Qur'ani, ufahamu na sayansi ya kitabu hicho imefanyika Novemba 18 katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran.
Hussein Asadi Mkurugenzi wa Masuala ya Qur’ani na Hadithi katika chuo hicho amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa, ‘awamu hii ya mashindano ilikuwa na wanachuo wa kidini elfu mbili raia wa kigeni. Mashindano hayo yamefanyika katika Kituo cha Elimu cha Imam Khomeini RA.
Ameongeza kuwa mitihani simulizi ya mashindano hayo pia imepangwa kwa ajili wanachuo wa Qur’ani katika kiwango cha shahada ya uzamivu (PhD), shahada ya uzamili (Master's), shahada ya kwanza na diploma. Amesema vyanzo vya mitihani hiyo vitakuwa vitabu vifuatavyo: “Maadili katika Mfumo wa Kiislamu” cha Ayatullah Subhani, “Tafsir Nemuneh” na Tafsiri ya Sura Anfal ya Hujjatul Islam Qaraati.
Mashindano ya Sayansi za Qur’ani yatakuwa katika msingi wa kitabu cha “Sayansi za Qur’ani” cha Hujjatul Islam Sa’eedi Rooshan na kitabu cha Ayatullah Ma’refat.
Fainali ya kitengo cha simulizi itafanyika mwezi Februari mwakani kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ambapo wanachuo wa kidini kutoka nchi 72 watashiriki.
Wanachuo 4000 kati ya elfu 10 kutoka maeneo mengine ya dunia wamejisajili kushirikia katika Olimpiadi hii. Wanachuo 200 watatunukiwa zawadi katika fainali. 900420
captcha