IQNA

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani kufanyika Qatar

13:43 - November 20, 2011
Habari ID: 2225151
Duru za sita ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Qatar yenye anwania ya 'Sheikh Ghanim bin Ali Athani' yataanza Disemba Mosi mwaka huu nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la As Sharq chapa ya Qatar, mashindano hayo yatajumuisha wanafunzi 1625 wakiwemo wavulana na washichana kutoka vituo vya Qur'ani nchini humo. 1056 kati yao ni wanafunzi kutoka vyuo vya kuhifadhi Qur'ani vinavyosimamiwa na Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu nchini Qatar.
Wanaoshirki katika mashindano hayo wanaendelea kujisajilisha. Mashindano hayo yanatazamiwa kuendelea kwa muda wa siku tatu.
901290
captcha