Mkuu wa Jihadi ya Vyuo Vikuu nchini Iran na wataalamu kadhaa wa kiuchumi wamehudhuria sherehe hiyo.
Katika mwaka huu ambao Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja kuwa 'Mwaka wa Jihadi ya Kiuchumi' nchini Iran, IQNA imeamua kuzindu kitengo cha kiuchumi.
Kitengo hiki cha habari kitakuwa cha kwanza kushughulikia masuala ya kiuchumi kwa mtazamo wa Kiislamu nchini Iran.
Shirika la Habari la Qur'an la Iran IQNA ndio la kwanza la pekee ambalo linashughulikia kwa njia maalumu habari za Qur'an katika ulimwengu wa Kiislamu. Juhudi zetu daima zimekuwa ni kusambaza habari na ripoti za Iran na ulimwengu mzima kwa ujumla kuhusu masuala yanayohusiana na Qur'ani Tukufu pamoja na habari kisiasa, kitamaduni, kisanaa, kiuchumi, kijamii vijana na watoto pamoja na kuzitathmini kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu.
902073