IQNA

Mashindano ya Qur’ani ya wanawake Canada

16:13 - November 23, 2011
Habari ID: 2227591
Mashindano ya kwanza kabisa ya Qur’ani maalumu kwa wanawake yamefanyika Novemba 20 huko Toronto, Canada.
Kwa mujibu wa Shirika la Utamaduni wa Ushirikiano wa Kiislamu la Iran (ICRO), mashidano hayo yalifanyika kwa ushirikiano wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Canada, Taasisi ya Kiislamu ya Imam Reza AS na taasisi zingine 15 za Kiislamu mjini humo.
Kituo cha Kiislamu cha Maasumin cha Toronto ndio kilichokuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya hifdhi na qiraa ya Qur’ani.
Wanawake 80 raia wa Canada na nchi kama Iran, Afghanistan na Pakistan walishiriki katika mashindano hayo.
Washindi walipata zawadi za fedha na Qur’ani za dijitali.
903469
captcha