IQNA

Kikao cha kuratibu mashindano ya kitaifa ya Qur'ani chafanyika Dubai

20:16 - November 23, 2011
Habari ID: 2227933
Kikao cha kuratibu na kupanga mashindano ya kitaifa ya Imarati Tuzo ya Dubai kilifanyika jana katika mji wa Dubai.
Shirika la habari la Imarati limeripoti kuwa lengo la kikao hicho lilikuwa kuchunguza mabadiliko yaliyofanyika katika mashindano hayo kama masharti na sifa za washiriki, vitengo vyake na kamati ya majaji.
Ahmad Saqar al Suwaidi ambaye ni mjumbe wa kamati inayosimamia mashindano hayo amesema kuwa wasimamizi wa mashindano hayo wanashirikiana na vituo vya Qur'ani vya Umoja wa Falme za Kiarabu katika kuchunguza njia za kuyaboresha zaidi.
Kikao cha kuratibu mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Tuzo ya Dubai kimewashirikisha wawakilishi wa vituo vyote vya Qur'ani nchini Imarati. 903824

captcha