Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe hiyo ilianza kwa kisomo cha Qur’ani Tukufu na kufuatiwa na ripoti iliyotolewa na Saniepur, katibu wa tamasha hiyo.
Wengine waliozungumza katika hafla hiyo ni Naibu Waziri wa Elimu, Naibu Waziri wa Utamaduni na Mkuu wa Kituo cha Kuratibu, Kustawisha na Kueneza Harakati za Qur’ani nchini Iran.
Tamasha hiyo ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Ferdowsi mjini Mash'had kuanzia tarehe 23 Novemba na ilijumuisha pia mashindano ya Qur’ani Tukufu.
904719