IQNA

Msikiti wa kale Uganda kukarabatiwa

22:28 - November 27, 2011
Habari ID: 2229986
Msikiti uliojengwa Uganda mwaka 1844 wakati Mflame Mutesa wa Kwanza aliposilimu utakarabatiwa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA tawi la Afrika, wafadhili kutoka Uturuki wamesema wataukarabati msikiti huo.
Imamu wa msikiti huo Nsimbi Ali Rajab amesema kuwa Uislamu uliingia Uganda mwaka 1840 na kuongeza kuwa Mfalme Mutesa wa Kwanza aliikubali dini tukufu ya Kiislamu na kuamuru msikiti huo ujengwe katika eneo la Kasubi mwaka 1844.
Hata hivyo katika kipindi cha miongo kadhaa sasa msikiti huo wa kale uliharibika, amesema Rajab, na kuongeza kuwa wafadhili wa Uturuki wameafiki kuukarabati na hivi karibuni utaanza kutumiwa na Waislamu kwa ajili ya kusimamishia Sala.
905899
captcha