IQNA

16:36 - November 29, 2011
Habari ID: 2231117

Vipindi vya Maisha ya Imam Hussein AS kutangazwa Redio Maarifa, Tanzania

Idhaa ya Maarifa nchini Tanzania imesema itatangaza vipindi maalumu kila siku katika mwezi wa Muharram kuhusu maisha ya Imam Hussein AS.

Taarifa il;iyotolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha Redio Maarifa Abubakr Amin amesema kuwa Redio Maarifa 105.3 FM iliyo katika mji wa Tanga, ndio redio ya kwanza ambayo inatangaza ujumbe wa Ahlul Bayt AS nchini Tanzania.
Bw. Amin ametoa wito kwa wale wenye uwezo kufadhili vipindi katika mwezi huu wa Muharram. Amesema gharama ya kila kipindi cha saa moja ni takribani 75,000 Tsh.
Bw. Amin amesema kuwa redio hiyo inawafikia wasikilizaji milioni moja na nusu katika eneo la pwani Tanzania. Ameongeza kuwa Idhaa hiyo itarusha vipindi vya mwezi wa Muharram chini ya anwani ya 'Eneza Ujumbe wa Imam Hussein Kupitia Redio Maarifa Tanzania'.
907633
captcha