IQNA

16:15 - December 10, 2011
Habari ID: 2235475

Ayatullah Sistani akataa kuonana na Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu

Ayatullahil Udhma Ali Sistani, marjaa mwandamizi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia mwenye makao yake nchini Iraq amekataa ombi la Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Nabeel al Arabi la kukutana naye.

Al Arabi aliyekuwa safarini nchini Iraq alitaka kumuona kiongozi huyo wa Waislamu wa Iraq lakini ofisi ya Ayatullah Sistani imesema amekataa ombi hilo, imeripoti tovuti ya Sawt al Iraq.
Akiwa Baghdad, Al Arabi amekutana na Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al Maliki, Waziri wa Mambo ya Nje Hoshyar Zebari na Spika wa Bunge Osama al Nujaifi.
Weledi wa mambo ya kisiasa wanasema Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imekuwa ikishirikiana na utawala wa Aal Khalifa wa Bahrain katika kuwakandamiza raia wanaoandamana kutaka demokrasia nchini humo. Aidha jumuiya hiyo ya nchi za Kiarabu imeonyesha misimamo ya kinafiki kuhusu kadhia ya Syria jambo ambalo linaashiria kushirikiana jumuiya hiyo na madola ya kibeberu ya nchi za Magharibi.
912183
captcha