IQNA

Kongamano la Kimataifa la 'Halal' kufanyika Pakistan

15:23 - December 11, 2011
Habari ID: 2236528
Kongamano la Pili la Kimataifa na Maonyesho ya Vyakula Halali yatafanyika Pakistan kwa ushirikiano wa utawala wa Jimbo la Punjab na Baraza la Utafiti wa Bidhaa Halali.
Kongamano hilo litafanyika Januari 16-17 katika mji wa Lahore nchini Pakistan ambapo lengo lake ni kuangazia umuhimu wa kutumia chakula halali katika Uislamu.
Hivi sasa kote duniani Waislamu wanazingaia sana suala la kutumia vyakula halali na hivyo mashirika mengi yanatilia mkazo suala la kupata cheti cha uzalishaji vyakula halali. Katika siku ya kwanza ya kongamano hilo masuala yatakayojadiliwa ni pamoja na uzoefu wa kimataifa katika sekta ya bidhaa halali, sekta ya bidhaa halali nchini Pakistan, utafiti wa bidhaa halali na utoaji vyeti na viwango vya bidhaa halali.
Katika siku ya pili washiriki watajadili kuhusu maabara ya kufanyia majaribio bidhaa halali katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Wanyama mjini Lahore, kichinjio cha nyama halali, nk.
913354
captcha