Kwa mujibu wa shirika la habari la Kuwait KUNA, Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa OIC amesema kwamba kuendelea miradi ya ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Wapalestina ni jambo linalokwenda kinyume na sheria za kimataifa pamoja na maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu huyo pia amelaani vikali shambulio lililofanywa na askari wa Kizayuni hivi karibuni katika msikiti mmoja katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan shambulio ambalo lilipelekea kuteketea sehemu ya msikiti huo.
Ekmeleddin Ihsanoglu amesema utawala wa Kizayuni unapasa kubeba jukumu la matukio hayo yote ya kichokozi dhidi ya Waislamu wa Palestina. Vilevile ameitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati mara moja na kuzuia kuendelea kwa siasa za mabavu na uchokozi za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wasio na hatia. 913416