IQNA

Wazayuni waendelea kuchoma misikiti Quds Tukufu

18:41 - December 14, 2011
Habari ID: 2238914
Walowezi wa Kizayuni mapema leo Jumatano wamechoma moto msikiti mmoja katika mji makatifu wa Quds.
Wazayuni hao walishambulia msikiti huo ulioko kaskazini mwa mji wa Quds wakaharibu sehemu moja ya eneo hilo la ibada na kuandika maneno yanayowavunjia heshima Waislamu katika kuta zake.
Kikosi cha zima moto kilikwenda haraka katika eneo hilo la kuzuia kuteketea kabisa msikiti huo ambao chumba chake kimoja kimeungua.
Walowezi wa Kizayuni wa Israel hadi sasa wamechoma moto misikiti na vituo vingi vya ibada vya Wakristo na Waislamu katika ardhi za Palestina zilizovamiwa na Israel mwaka 1948 na katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Mashambulizi hayo yamekuwa yakiungwa mkono na viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na taasisi rasmi za utawala huo ghasibu. 915807
captcha