Tovuti ya al Manar imeripoti kuwa Taasisi ya al Aqsa imetoa taarifa ikisema kuwa hatua hiyo si ya kisheria na inavunjia heshima Msikiti wa Biir Sabi ambao ni sehemu ya ibada ya Waislamu. Imesisitiza kuwa sehemu hiyo ni wakfu wa Kiislamu na hakuna mtu au upande wowote wenye mamlaka ya kubadili matumizi ya eneo hilo.
Taarifa ya Taasisi ya al Aqsa imeendelea kusema kuwa msikiti huo ulijengwa mwaka 1908 wakati wa utawala wa Othmania na kundi lolote lisilokuwa na Waislamu halina haki ya kuutumia.
Taarifa ya Taasisi ya al Aqsa imemalizia kwa kusema: Awali taasisi hii ilipinga hukumu iliyotolewa na mahakama moja ya utawala ghasibu wa Israel ya kubadili msikiti huo na kuufanya jumba la makumbusho. Imesisitiza kuwa Msikiti wa Biir Sabi ni wakfu wa Kiislamu na wananchi wa Palestina hawataruhusu utumiwe kwa ajili ya kazi nyingine zisizokuwa za ibada. 924758