IQNA

15:58 - January 04, 2012
Habari ID: 2251012

Utawala wa Kizayuni uzuiwe kuyahudisha Quds Tukufu

Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) Ali Larijani ametuma ujumbe kwa maspika wenzake kote duniani akisisitiza umuhimu wa kuchukuliwa hatua za kivitendo dhidi ya hatua ya bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel kutangaza Quds (Jerusalem) kama mji mkuu wa utawala huo.

Katika ujumbe wake, Larijani amesema, ‘Historia ya Palestina inaonyesha kuwa utawala wa Kizayuni, kutokana na msingi wake wa kichokozi, daima umekuwa ukijaribu kutumia kila fursa kuteka ardhi zaidi za Palestina na kulazimisha sera zake zilizo kinyume cha ubinadamu dhidi ya watu madhlumu wa Palestina’.
Ameongeza kuwa kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya hujuma za Wazayuni dhidi ya matukufu ya Kiislamu na Kikristo katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ni jambo ambalo limelipa kiburi bunge ya utawala wa Kizayuni kutafakari mpango wa kuufanya mji wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala bandia wa Israel.
Larijani amesema kuwa Jamuri ya Kiislamu ya Iran, kwa msingi wa misimamo yake imara isiyotetereka dhidi ya utawala haramu wa Israel, inalaani njama za kuutangaza mji wa Quds kuwa mji mku wa utawala bandia wa Israel.
Naye Ali Akbar Salehi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Israel ni chanzo cha matatizo yote katika eneo la Mashariki ya Kati na kwamba utawala wa Kizayuni umejengeka juu ya misingi ya uchochezi na kuleta migawanyiko. Salehi ameyasema hayo hapa mjini Tehran katika mazungumzo kati yake na Muray Yildirim Mkuu wa kundi la urafiki wa kibunge kati ya Uturuki na Palestina.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amelaani pia ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kuitaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kutimiza wajibu wake katika uwanja huo. Salehi amesisitiza kuwa muqawama ni njia pekee itakayowawezesha Wapalestina kupata haki zao. Aidha amesema kuwa nchi za Magharibi zinajaribu kuzidisha mashinikizo kwa Iran ili kukwamisha maendeleo ya taifa hili.
928220
captcha