Makumi ya walowezi wa Kizayuni jana usiku walishambulia vijiji vya Burin na Iraq Burin huko kusini mwa Nablos na kupigana na wanavijiji na askari wa eneo hilo.
Afisa anayeshughulikia faili la ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni Ghassan Daghlish amesema kuwa walowezi wa Kizayuni wa eneo la Bracha wamevamia kijiji cha Burin na kuvunja vioo vya madirisha ya nyumba na kupigana na wanakijiji hicho.
Amesema kuwa askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel pia wameshirikiana na walowezi hao kwa kuwafyatulia risasi na gesi ya kutoa machozi wanakijiji wa Palestina. Askari hao pia walizuia magari ya wagonjwa kuingia katika kijiji hicho kwa ajili ya kusaidia majeruhi. 930968