IQNA

11:30 - January 12, 2012
Habari ID: 2255779

ISESCO yalaani Israel kwa kuchapishaji picha ya Al Aqsa bila Qubat As-Sakhra

Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO limelaani vikali hatua ya jeshi la utawala haramu wa Israel kuchapisha picha ya Msikiti Mtakatifu wa Al Aqsa bila Qubat As Sakhra.

Tarifa ya ISESCO imesema kuchapishwa picha hiyo kuna weka wazi malengo halisi ya utawala ghasibu wa Israel ambayo ni kuuyahudisha mji wa Quds na kuubomoa Msikiti wa Al Aqsa na kujenga mahala pake hekalu la Kiyahudi.
ISESCO imeonya kuhusu njama za Wazayuni kubomoa Qibla cha kwanza cha Waislamu na vilevile njama za kubomoa maeneo mengine ya kidini ya Kiislamu na Kikristo huko Quds. Imesema njama hizo za utawala wa Kizayuni wa Israel huenda zikaibua vita vya kidini katika eneo la Mashariki ya Kati.
ISESCO pia imetoa wito kwa jamii ya kimataifa na mashirika husika kuchukua hatua za haraka kulinda haki zilizotambulika za kihistoria za Waislamu na Wakristo katika mji wa Quds.
Shirika hilo limesema matukufu ya Kiislamu na Kikristo huko Quds ni mstari mwekundu usioweza kupitwa.
933260
captcha