Kwa mujibu wa tovuti ya CPI, kamati hiyo imeashiria amri ya hivi karibuni ya utawala huo haramu ya kujenga sehemu ya kuegezea magari katika eneo la Waarmania huko Quds na kuongeza kuwa utawala huo umekuwa ukibomoa nyumba na makaazi ya Waislamu na Wakristo katika eneo hilo kwa lengo la kuwalazimisha walihame.
Katika taarifa hiyo utawala wa Kizayuni umekosolewa vikali kwa kupora wakfu za Waislamu na Wakisto kwa lengo la kuufanya mji mtakatifu wa Quds kuwa wa Mayahudi.
Katika hatua yake ya kichokozi ya hivi karibuni kabisa, utawala wa Israel umepora ardhi za Waarmania katika eneo la zamani la Quds na kuwapa walowezi wa Kizayuni.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas pia jana ilitoa taarifa ikilaani vikali kitendo hicho cha utawala haramu wa Israel. 949090