IQNA

Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Nasrullah:

Bila ya misaada ya Iran, ushindi dhidi ya Israel usingepatikana

17:04 - February 08, 2012
Habari ID: 2271485
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa ingekuwa muhali harakati hiyo kupata ushindi dhidi ya utawala ghasibu wa Israel bila ya kupata misaada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran umeleta umoja wa Kiislamu.
Sayyid Hassan Nasrullah ameashiria vita vya miaka minane dhidi ya Iran vilivyoungwa mkono na Marekani, Israel na hata baadhi ya nchi tajiri za Kiarabu na kueleza kuwa fedha za nchi za Kiarabu badala ya kutumiwa kusaidia mapambano ya kuikomboa Palestina na Quds Tukufu, zilitumika katika kuunga mkono vita dhidi ya Iran.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameyasema hayo jana usiku katika sherehe za kukumbuka siku ya kualiwa Mtume Mtukufu wa Uislamu Muhammad al-Mustafa S.A.W zilizohudhuriwa na maelfu ya raia wa Lebanon sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Umoja huko kusini mwa Beirut. Nasrullah amepongeza misaada ya Iran kwa harakati ya mapambano ya Hizbullah khususan katika vita ya siku 33 vilivyoanzishwa na Israel dhidi ya Lebanon, ambapo utawala haramu wa Kizayuni ulipata pigo kali. Amesema muqawama huko Lebanon umepata mafanikio makubwa sana dhidi ya Israel na kwamba hilo lisingeweza kutimia bila ya msaada wa Iran.
Sayyid Hassan Nasrullah amewatolea mwito Waislamu kuwa na umoja na kukosoa pia njama zinazofanywa kwa lengo la kutaka kuharibu taswira ya Iran katika eneo. 949799
captcha