Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah:
Vita laini, changamoto kubwa zaidi inayowakabili Waislamu
Umma wa Kiislamu haukabiliwi na mashamabulizi ya kijeshi bali mashambulizi ya kiutamaduni, kijamii na kiuchumi, na kwa hakika vita laini ndio changamoto kubwa zaidi inayowakabili Waislamu katika zama hizi.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naeem Qasim katika sherehe za kufunga mashindano ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu iliyofanyika jana mjini Beirut. Ameongeza kuwa changamoto kubwa zaidi inayoukabili Umma wa Kiislamu ni vita vya vyombo vya habari au vita laini ambavyo vinaingia majumbani mwetu na kuathiri watu wa familia kupitia vyombo vya habari.
Sheikh Qasim amesisitiza kuwa vitisho vya kuishambulia kijeshi Iran na Syria vinavyotolewa na Marekani na Israel ni sehemu ya siasa za kuzusha hofu na woga za mabeberu hao. Amesema njia pekee ya kuwashinda mabeberu hao ni mapambano na kusimama kidete. 952231