IQNA

16:09 - February 15, 2012
Habari ID: 2274596

Kongamano la pili la wanazuoni wa Kishia na Kisuni kufanyika Hamburg

Kongamano la pili la wanazuoni wa Kishia na Kisuni limepangwa kufanyika tarehe 18 Februari katika Kituo cha Kiislamu cha Hamburg nchini Ujerumani.

Kwa mujibu wa idara ya uhusiano wa umma ya kituo hicho, kongamano hilo litafanyika kwa mnasaba wa Wiki ya Umoja wa Kiislamu chini ya anwani ya 'Sira ya Mtume Mtukufu (saw) na Nafasi ya Zama na Sehemu.'
Kongamano hilo litajadili sira ya Mtume na mafundisho yake katika zama na sehemu anayoishi mwanadamu wa sasa pamoja na athari zake kwa harakati na mwamko wa Kiislamu unaoshuhudiwa katika pembe tofauti za dunia.
Washiriki wa kongamano hilo watajadili namna sira na mafundisho ya Mtume yanaweza kutumiwa katika kukabiliana na changamoto tofauti zinazowakabili wanadamu katika ulimwengu wa leo na hasa wa Kiislamu.
Ayatullah Ridha Ramadhani, Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Hamburg, Hujjatul Islam wal Muslimin Rasul Jaafariyyan, Mtafiti mashuhuri wa historia ya Kiislamu, Profesa Ilham Gular, mwandishi na mhadhiri wa vyuo vikuu vya Uturuki pamoja na wasomi na wanachuo mashuhuri wa Kishia na Kisuni wa nchini Ujerumani wamealikwa kushiriki na kuzungumza katika kongamano hilo. 953352
captcha